Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Serikali yakamata Mzigo wa Maana wa Tanzanite Ukitoroshwa nje

Serikali yakamata Mzigo wa Maana wa Tanzanite Ukitoroshwa nje

Picha
Serikali imefanikiwa kuyakamatwa madini ya Tanzanite yenye thamani ya Sh2.5  bilioni yaliyokuwa njiani kusafirishwa nje ya nchi bila kulipiwa vibali kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana.  Hayo yameelezwa leo jijini hapa na Kaimu Kamishna wa madini nchini, Mhandisi Ally Namaje wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya tatu ya kimataifa ya madini ya Vito yanayofanyika jijini hapa.  Mhandisi Namaje amesema madini hayo yaliyokuwa na uzito wa Kilo  mbili ni sehemu tu ya madini yanayoendelea kutoroshwa na watanzania wasiokuwa wazalendo na nchi yao lakini hata hivyo Serikali inaendelea kuziba mianya yote ya utoroshwaji wa madini hayo nje ya nchi.  "Sheria inasema baada ya madini hayo kukamatwa tunayataifisha na kuyauza kwa mnada, kwa hiyo katika maonyesho haya tutayauza katika mnada wa hadhara ili kila mtu mwenye uwezo aweze kununua," amesema Namaje.  Amesema pia katika kipindi hicho wizara yake imefanikiwa kukamata madini ya Dhahabu yakiwa njiani kutoroshew...