Iran na Singapore kustawisha ushirikiano baina yao
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Singapore wamejadili na kubadilishana mawazo juu ya kustawisha uhusiano wa nchi mbili katika nyuga tofauti za kiuchumi na vilevile juu ya masuala ya kieneo.Katika mazungumzo aliyofanya mapema leo na Waziri mwenzake wa Singapore Vivian Balakrishnan huko mjini Singapore, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Muhammad Javad Zarif ameashiria fursa na uwezo wa kiuchumi wa Iran na kuhuika ushusiano wa nchi za Asia na Tehran katika kipindi cha baada ya kuondolewa vikwazo, na kueleza kwamba Iran inakaribisha kuhuisha uhusiano na Singapore katika nyanja tofauti za kiuchumi hususan za nishati, benki, usafiri wa baharini, elimu, afya, teknolojia ya habari, petrokemikali na uwekezaji vitega uchumi.Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore Vivian Balakrishnan ameeleza kufurahishwa na safari iliyofanywa na ujumbe wa ngazi za juu wa nchi yake hapa mjini Tehran na kusainiwa hati za makubaliano katika sekta ya uwekezaji vitega uchumi baina ya nchi hizo mbili na ...