Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Singapore wamejadili na kubadilishana mawazo juu ya kustawisha uhusiano wa nchi mbili katika nyuga tofauti za kiuchumi na vilevile juu ya masuala ya kieneo.Katika mazungumzo aliyofanya mapema leo na Waziri mwenzake wa Singapore Vivian Balakrishnan huko mjini Singapore, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Muhammad Javad Zarif ameashiria fursa na uwezo wa kiuchumi wa Iran na kuhuika ushusiano wa nchi za Asia na Tehran katika kipindi cha baada ya kuondolewa vikwazo, na kueleza kwamba Iran inakaribisha kuhuisha uhusiano na Singapore katika nyanja tofauti za kiuchumi hususan za nishati, benki, usafiri wa baharini, elimu, afya, teknolojia ya habari, petrokemikali na uwekezaji vitega uchumi.Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore Vivian Balakrishnan ameeleza kufurahishwa na safari iliyofanywa na ujumbe wa ngazi za juu wa nchi yake hapa mjini Tehran na kusainiwa hati za makubaliano katika sekta ya uwekezaji vitega uchumi baina ya nchi hizo mbili na kuongeza kuwa Singapore ina hamu ya kushirikiana na kuwekeza pamoja na Iran katika nyuga mbalimbali hususan petrokemikali.Dakta Zarif amekutana na kufanya mazungumzo pia na Tharman Shanmugaratnam, Naibu Waziri Mkuu anayehusika na masuala ya uchumi ambaye pia ni Gavana wa Benki Kuu ya Singapore na kubadilishana mawazo juu ya ushirikiano wa nchi mbili katika sekta za uchumi na benki.Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliwasili nchini Singapore jana usiku na kulakiwa na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wa nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia.../