SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 8 Machi 2016

T media news

ya Trump yawatia wasiwasi wanadiplomasia wa kigeni walioko Marekani

Wanadiplomasia wa kigeni walioko Marekani wamewalalamikia baadhi ya maafisa wa serikali ya nchi hiyo kuhusiana na matamshi ya uzushaji fitna na ya matusi ya Donald Trump, mwanasiasa wa Chama cha Republican anayeongoza katika kampeni za kuwania uteuzi wa kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho.Kwa mujibu wa maafisa waandamizi wa serikali ya Marekani, katika mazungumzo ya faragha waliyofanya hivi karibuni na maafisa wa nchi za Ulaya, Mashariki ya Kati, Asia na Amerika ya Latini, maafisa wa nchi hizo walieleza kwamba wanatiwa wasiwasi na matamshi ya chuki dhidi ya wageni yanayotolewa na Trump.Maafisa watatu waandamizi wa serikiali ya Washington ambao hawakutaka kutajwa majina yao wamesema wanadiplomasia hao wa kigeni walionyesha kukerwa na kuchukizwa na misimamo dhidi ya Uislamu na dhidi ya wahajiri ya mwanasiasa huyo.Bila ya kutaja orodha kamili ya nchi husika, maafisa hao wamezitaja Mexico, Korea Kusini, Japan na India kuwa ni miongoni mwa nchi ambazo wanadiplomasia wao wamelalamikia matamshi ya Donald Trump.Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani si jambo la kawaida hata kidogo kwa wanadiplomasia wa kigeni kuonyesha kuwa na wasiwasi na mgombea wakati wa hekaheka za kampeni za uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.Viongozi wa nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Canada, Ufaransa na Mexico, wameshajitokeza hadharani kukosoa misimamo ya Trump. Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alinukuliwa mwezi Januari mwaka huu akisema:"kwa maoni yangu, sio tu matamshi ya Trump ni ghalati lakini pia yanaifanya kazi yetu ya kuwadhibiti na kuwashinda watu wenye misimamo ya kufurutu mpaka iwe ngumu zaidi".../