Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Barabara ya Mwenge hadi Morocco Iliyojengwa Kwa Fedha za Sherehe za Uhuru Yakamilika kwa asilimia 95

Barabara ya Mwenge hadi Morocco Iliyojengwa Kwa Fedha za Sherehe za Uhuru Yakamilika kwa asilimia 95

Picha
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa  amekagua  mradi wa upanuzi wa barabara ya Mwenge  hadi Morocco yenye kilomita 4.3 ambapo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 95.   Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara hiyo  Prof.Mbarawa ameeleza kuwa tayari njia tano zimeanza kutumika kuanzia eneo la Mwenge hadi Kijitonyama zenye urefu wa  kilomita 2 huku kilomita nyingine 2.3 zikiwa katika harakati za mwisho za kukamilishwa.   “Serikali imedhamiria katika kuhakikisha kuwa  inatatua kero ya  msongamano wa magari kwa kufanya upanuzi wa njia  muhimu ili kurahisisha hali ya usafiri jijini Dar es Salaam ”  alisema Prof.Mbarawa.   Aliongeza kwa kusema hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli alizindua mradi wa daraja la Kigamboni linalounganisha kurasini na Kigamboni pamoja na kuweka  jiwe la msingi  kwa a...