YANGA SC imefanikiwa kwenda hatua ya makundi
Na Prince Akbar, DUNDO YANGA SC imefanikiwa kwenda hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika licha ya kufungwa bao 1-0 na wenyeji Sagrada Esperanca jioni ya leo Uwanja wa Esperanca mjini Dundo, Angola. Kwa matokeo, hayo Yanga inakwenda hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 2-1, baada ya awali kushinda 2-0 Dar es Salaam, mabao ya Simon Msuva na Matheo Anthony. Matokeo hayo si tu yanamaanisha Yanga inatinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza katika historia yake, bali pia inakuwa timu ya kwanza ya Tanzania kufika hatua hiyo ya michuano hivyo. Kikosi cha Yanga kilichoanza leo mjini Dundo, Angola Awali ya hapo, Yanga imewahi kuwa timu ya kwanza ya Tanzania kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1998, ikafuatiwa na mahasimu, Simba SC mwaka 2003. Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na marefa wa Madagascar, Hamada el Moussa Nampiandraza, aliyesaidiwa na Velomanana Ferdinand Jinoro na J...