Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Drake

Diamond Kwenye Headlines Nyingine Na Wizkid, AKA, Drake, Beyonce na Rihanna

Picha
May 20 2016  Tanzania imeamka na habari nyingine njema za Diamond Platnumz kuchaguliwa tena kushiriki kwenye tuzo za kituo maarufu cha TV Marekani kiitwacho  BET  ambapo Platnumz amekua na mwaka mwingine mfululizo wa kuwa nominated na sasa ni kwenye tuzo za  BET Awards 2016. Diamond ameshukuru kwa kuchaguliwa kuwania tuzo kwenye kipengele cha Best international Act Africa ambapo ameyaandika maneno haya baada ya kufikiwa na taarifa >>> ‘ Ningependa niwashukuru kwa Sapoti kubwa Manayozidi kunipa na niwajuze kuwa kijana wenu nimechaguli kuwania tunzo ya Msanii Bora wa Kimataifa toka Africa kwenye tunzo za BET  #BETAwards America’ Tuzo za BET 2016 ambazo zitatolewa nchini Marekani zimeanza kuchukua nafasi kwenye headlines baada ya kutangazwa list ya waliochaguliwa kuwania huku  Beyonce ,  Rihanna  na Drake  wakitangazwa kuongoza kwa kuwania tuzo zaidi ya moja.