JPM: Bakwata liombeeni taifa

RAIS John Magufuli amewahimiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), kuendelea kuombea amani katika taifa na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii.

Kauli hiyo ya Rais ilitolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, kwa niaba ya Rais katika futari iliyoandaliwa na Bakwata katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim, Dar es Salaam.

Rais Magufuli alisema jamii yoyote, inayolelewa na kukua katika misingi ya kufuata maandiko ya Mungu ni vigumu kujiingiza katika vitendo vinavyomchukiza Mungu, vikiwemo vya uhalifu.

Alisema Rais Magufuli amewatakia heri waumini wote wa dini ya kiislamu kote nchini katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa upande wake, Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar Zubeir, aliipongeza serikali kwa hatua inazochukua katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu nchini na kusisisita kuwa viongozi wa Bakwata, wataendelea kushirikiana na serikali katika kukemea vitendo viovu katika jamii, kama hatua ya kuhakikisha vitendo vya uhalifu vinakoma nchini.

Alitoa rai kwa waislamu wote nchini, kudumisha umoja, upendo na mshikamano miongoni mwao katika mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na hata baada ya mfungo huo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA