SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 30 Aprili 2016

T media news

GEITA GOLD MINE FC YATWAA NAFASI YA PILI MICHUANO YA MEI MOSI 2016

Geita Gold Mine Football Club imetangazwa mshindi wa pili wa michuano ya Mei Mosi (May Day) baada ya kufungwa kwa magoli 2-0 dhidi ya Halmashauri ya mkoa wa Geita.

Maneja wa timu ya Geita Gold Mine FC Mikidadi Suleiman amsema ameridhishwa na kiwango cha soka kilichooneshwa na wachezaji wake licha ya kupoteza mchezo wao.

Amesema wamepoteza mchezo dhidi ya timu bora lakini wanaendelea kujiandaa kwa ajili ya michuano mingine ijayo.

Tulifanya kila tuwezalo kwenye michuano hii, haikuwa rahisi kuIfunga TANESCO FC siku ya Jumanne na kutinga hatua ya fainali. Tulipambana na hatimaye kuichapa TANESCO kwa penati 4-2 na kufika hatua ya fainali ambayo ilikuwa ni muhimu kwetu”, amesema Suleiman na kuongeza kuwa, kama kikosi chake kisingekuwa na majeruhi wengi, wangefanikiwa kutwaa kombe la mashindano.

Golikipa wa Geita Gold Mine Football Club Emanuel Charles amesema timu bora ilistahili kutwaa ubingwa.

“Tulicheza kama timu kipindi cha kwanza lakini mabeki wangu hawakutimiza majukumu yao kuzuia mashambulizi golini kwetu. Ilikuwa ni kosa kubwa kuruhusu goli la kwanza dakika ya nne kabla ya kuruhusu goli la pili dakika 10 kabla ya half-time”.

Maneja rasilimali watu (HR) wa Geita Gold Mine FC amesema, timu yao kufika hatua ya fainali inadhihirisha kwamba ni mabingwa pia.

“Kulikuwa na timu nyingi kwenye mashindano haya. Kuwa washindi wa pili si kitu rahisi. Tumeliwakilisha vema jina la Geita Gold Mine Company. Sasa tunajiandaa kwa mashindano mengine”.