SIMBA YAMUWASHIA KESSY TAA YA KIJANI KWENDA ANAKOTAKA
Ramadhani Kessy-Beki wa Simba SC
Uongozi wa Simba umemuwashia taa ya kijani beki wake wa kulia Hassan Kessy baada ya nyota huyo kusema hatoendelea kutoa huduma yake kwenye klabu hiyo baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa golikipa wake Mu-Ivory Coast Vicent Agban baada ya Kessy kutolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu wakati wa mchezo wa VPL kati ya Simba dhidi ya Toto Africans.
Afisa habari wa klabu hiyo amekaririwa na kituo kimoja cha radio akisema Kessy ameikuta Simba na ataondoka na kuiacha hivyo kama ameamua kuondoka asubiri hadi mkataba wake utakapomalizika aachane na klabu hiyo.
“Sisi tunafahamu Kessy bado tunamkataba naye kama ataamua kuiacha Simba, Simba siyo ya babayake wala ya mamayake anaweza akaenda popote anapotaka tunamruhusu lakini atomize majukumu yake amalize mkataba wake, lakini kama kaamua hivyo sawa maisha yataendelea tu hata akiondoka Simba bado itaendelea kuwepo”, anasema Manara afisa habari wa klabu ya Simba SC.
Agban alimchapa makonde Kessy akimtuhumu kutumiwa na wapinzani wao wa jadi Yanga kuihujumu Simba kufuatia kuoneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Edward Christopher wa Toto Africans. Baada ya mchezo kumalizika golikipa huyo alimvaa Kessy na kuanza kumshushia kichapo.
Kessy anasema amekuwa kwenye wakati mgumu baada ya kusababisha goli kwenye mchezo dhidi ya Yanga ambapo pasi yake kuelekea kwa golikipa ilinaswa na mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma na kufunga bao.
Mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar anazidi kusema hayuko tayari kuichezea klabu ya Simba na mkataba wake utakapomalizika ataachana na klabu hiyo na kutafuta maisha sehemu nyingine.
Maoni
Chapisha Maoni