Azam yamaliza kazi wa Bidvest

Kocha msaidizi wa Azam, Mario Marinica amesema wameshaipeleleza vya kutosha klabu ya Bidvest WitsWachezaji wa Azam wakisikiliza ushauri wa kocha wao wa Mario Marinica wakati wa mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mbeya iliyofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Picha na MaktabaDar es Salaam. Kocha msaidizi wa Azam, Mario Marinica amesema wameshaipeleleza vya kutosha klabu ya Bidvest Wits watakayokutana nayo Jumamosi na kuahidi kuwa watapata ushindi.Azam itapambana na Bidvest Jumamosi nchini Afrika Kusini katika mchezo wa raundi ya kwanza ya  Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) utakaoanza saa 12:00 jioni.Marinica aliyekwenda Afrika Kusini kuitazama Bidvest ikiilaza Lightstars ya Shelisheli kwa mabao 6-0 katika mchezo wa nyubani ilishinda mchezo wa kwanza kwa mabao 3-0.Katika safari hiyo, kocha huyo aliongozana na  mwenzake, Dennis Kitambi aliyesema kazi imekamilika. Kocha huyo, raia wa Romania alisema wanatakiwa kumaliza tatizo la kushindwa kutumia vyema nafasi za kufunga mabao wanazotengeneza ili kuifanya kazi yao kuwa rahisi katika mchezo huo. Alisema wameiona Bidvest kwenye baadhi ya mechi zake na wanajua mbinu wanazotumia, hivyo watatumia udhaifu wa wapinzani wao kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.“Utakuwa mchezo mgumu kwani Bidvest ni timu nzuri na tayari tumeshawapeleleza kwenye mechi kadhaa, tunajua ubora wao na udhaifu wao, lakini sisi tumejipanga na tuko kamili kwa mapambano.“Sisi tuna kikosi bora, lakini tatizo kubwa tulilonalo katika timu yetu ni kushindwa kutumia nafasi tunazotengeneza za kufunga mabao jambo tunalotakiwa kulifanyia kazi kabla ya mchezo huo,” alisema Marinica.Baada ya mchezo huo, Azam itarudiana na  timu hiyo, Machi 20 jijini Dar es Salaam na mshindi atakutana na mshindi kati ya Renaissance ya Chad na Esperance ya Tunisia  Azam  imeanza moja kwa moja kwenye raundi ya kwanza ya Kombe la CAF wakati wapinzani wao, Bidvest wakianzia hatua ya awali kwa kuwatoa Lightstars ya Shelisheli kwa mabao 9-0 yaliyotokana na ushindi wa mabao 3-0 ugenini

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA