NYAMA NYEKUNDU NA ZA KUSINDIKWA ZINASABABISHA SARATANI YA TUMBO


Taasisi ya Shirika la Afya Duniani (WHO) inayohusika na tafiti juu ya saratani, IARC (The International Agency for Research on Cancer) ilifanya tafiti juu ya hatari ya saratani ya utumbo kutokana na matumizi ya nyama nyekundu na ya kusindikwa. Kabla ya hapo, nyama nyekundu na za kusindika zimekuwa zikihusishwa na saratani ya utumbo pamoja na magonjwa ya moyo na shinikizo la damu.

Maana Ya Nyama Nyekundu na Nyama Ya Kusindikwa
Nyama nyekundu ni nyama inayotokana na misuli ya wanyama aina ya mamalia kama ng’ombe, mbuzi, kitimoto, kondoo, swala, nyati, punda, mbwa, panya na kadhalika.

Nyama ya kusindika ni nyama iliyowekwa chumvi, kukaushwa, kuokwa kwa moshi au kemikali za kuisaidia kukaa muda mrefu bila kuharibika au kutopoteza ladha yake. Nyama ya kusindika inaweza kuwa ya ng’ombe, nguruwe, kuku, kondoo n.k. Baadhi ya nyama za kusindika ni kama hotdogs, ham, sausages, nyama za kopo n.k.

Matokeo ya utafiti huu uliotangazwa tarehe 26 Oktoba 2015 yanaonesha kuwa utumiaji wa nyama za kusindikwa una hatari ya kusababisha saratani ya utumbo wakati nyama nyekundu pia ikihusishwa na utokeaji saratani ya utumbo kwa kiasi fualani.

Ingawa kuna hatari, lakini nyama za kusindika zinaongeza uwezekano wa kupata saratani ya utumbo kwa kiasi kidogo. Inakadiriwa ulaji wa gramu 50 nyama za kusindika kwa siku unaongeza hatari ya saratani kwa asilimia 18%. Inakadiriwa zaidi ya vifo 34000 kila mwaka hutokea kutokana na magonjwa yanayotokana na ulaji wa nyama za kusindika.

Katika utafiti huu nyama za kusindikwa zipo kundi la 1 (carcinogenic). Hii inamaanisha kuna ushahidi wa kutosha wa kisayansi kuonesha nyama za kusindikwa zinasababisha saratani ya utumbo. Nyama nyekundu (red meat) imewekwa kwenye kundi la 2A katika hatari ya kusababisha saratani kwa binadamu. Hii inamaanisha kuwa nyama nyekundu inaweza kusababisha saratani ya utumbo kwa binadamu.

Nini kinafanya nyama nyekundu au ya kusindikwa kusababisha saratani?
Nyama nyekundu inapopikwa hutengeneza kampaundi za heterocyclic aromatic amines na polycyclic aromatic hydrocarbons. Pale nyama zinaposindikwa hutengeneza kemikali za kampaundi za N-nitroso na polycyclic aromatic hydrocarbons. Baadhi ya kampaundi hizi zinajuluikana au kuhisiwa kusababisha saratani (carcinogens).

Je, niache kula nyama?
Nyama ni sehemu muhimu ya mlo. Unaweza kula nyama ila kwa kiasi. Vizuri upunguze kiasi cha nyama nyekundu kwenye mlo wako, acha za kusindikwa na tumia zaidi nyama ya kuku au samaki. Ukiweza kuacha nyama nyekundu au nyama kwa ujumla ina faida kubwa zaidi kwa afya yako.

Kiasi gani cha nyama ni salama kula?
Mpaka sasa hakuna kiasi fulani cha nyama kilichothibitishwa kuwa ni salama kutumiwa kwa siku. Ila kadri unapokula nyama kwa wingi hasa ya kusindika ndivyo hatari ya kupata saratani inapoongezeka.

“uwezekano wa kupata saratani ya utumbo wa mtu kutokana na matumizi ya nyama za kusindikwa ni mdogo, lakini hatari hii huongezeka kadri kiasi cha nyama kinacholiwa kinapoongezeka” Kiongozi wa utafiti huo, Dr Kurt Straif alisema.

Matokeo ya utafiti huu yatatumika kwenye kuandaa mapendekezo ya lishe, miongozo na sera za kupunguza utokeaji wa saratani.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA