TATOA WAMPONGEZA JPM KWA BOMBA LA MAFUTA ...!!!


WASAFIRISHAJI nchini wamempongeza Raisi John Magufuli kwa juhudi zake zilizoiwezesha Tanzania kupata mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta litakalojengwa kutoka Uganda hadi Tanga.

Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) pia kimeipongeza timu ya mazungumzo iliyoongozwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, huku kikiwataka wanachama wake na wadau wote kwa ujumla kuchangamkia fursa nyingi na kubwa za kibiashara zitakazotokana na ujenzi wa bomba hilo.

“Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa rais wetu na timu iliyoshiriki kwenye mazungumzo, wametufanyia jambo kubwa katika ujenzi wa uchumi wa nchi...imebaki juu yetu kupanga mikakati ya namna ya kutumia fursa za kibiashara zitakazoletwa na mradi huu,” alisema Mwenyekiti wa Tatoa, Angelina Ngalula jijini Dar es Salaam jana.

Ngalula alisema kutokana na fursa hii kubwa iliyopatikana, wadau wote wa bandari wana wajibu wa kuitumia katika kutangaza bandari zilizopo nchini ili kuvutia wawekezaji na wateja katika kukuza uchumi wa nchi.

“Fursa hii kubwa itaifanya Bandari ya Tanga kuingia katika ramani ya dunia hivyo basi ni vyema wadau wote wa bandari na wapenda maendeleo kuitumia vizuri nafasi hii,” alisema mwenyekiti na kuongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,403 kutoka Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga utatengeneza fursa nyingi za usafirishaji mizigo kwa njia ya reli na barabara.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA