Pilikapilika za Israel kwa ajili ya kuanzisha vita vingine dhidi ya Gaza

Katika kuendeleza siasa zake za kupenda vita katika Mashariki ya Kati, utawala wa Kizayuni wa Israel umo katika maandilizi ya kuanzisha vita vingine dhidi ya Ukanda wa Gaza.Moshe Yaalon, Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema kuwa, utawala huo umo katika maandalizi ya kufanya shambulio jingine dhidi ya Ukanda wa Gaza huko Palestina. Moshe Yaalon ametoa vitisho hivyo dhidi ya Wapalestina akiwa katika meli ya kivita ya Marekani ya USS Carney ambayo kwa sasa ipo huko Haifa Palestina kwa ajili ya manuva ya kijeshi ya Israel na Marekani. Kushtadi vitisho vya viongozi wa Israel dhidi ya Wapalestina tena katika kipindi hiki ambacho utawala huo ghasibu unafanya luteka ya pamoja na Marekani ni jambo linaloonesha kuanza duru mpya ya pilikapilika za kijeshi za Israel katika Mashariki ya Kati ikishirikiana na Marekani, harakati ambazo zinaonesha kuendelea siasa za kupenda vita za utawala huo ghasibu. Vitisho vya Israel dhidi ya Gaza vinaendelea kutolewa katika hali ambayo, miaka ya 2008, 2012 na 2014 Israel ililishambulia eneo la Ukanda wa Gaza, ambapo licha ya mashambulio hayo kuwa makubwa na kupelekea pia kuuawa maelfu ya watu wasio na hatia, lakini viongozi wa Tel Aviv walishindwa kufikia hata lengo lao moja kupitia mashambulio hayo. Vitisho hivyo vinavyotolewa baada ya kufunuka pazia la utawala huo la kutaka amani kufuatia kukabiliwa na mkwamo mazungumzo eti ya mapatano, kwa mara nyingine tena vinazidi kuweka wazi sura halisi ya utawala huo haramu. Bila shaka jambo hili linabainisha kwamba, utawala huo ulio dhidi ya ubinaadamu hakuna wakati ambapo ulitaka amani katika Mashariki ya Kati. Ni dhahir shahir kwamba, kushindwa Israel kisiasa na kijeshi na muqawama wa wananchi katika eneo, ni jambo ambalo kivitendo limewafanya viongozi wa Tel Aviv waingiwe na wahaka na wasiwasi mkubwa. Ni kwa kuzingatia ukweli huo ndio maana sasa viongozi hao wameshadidisha harakati za kijeshi ili kwa njia hiyo wafunike kushindwa kwao.Ukweli wa mambo ni kuwa Israel imekuwa ikitumia kila fursa kwa ajili ya kusukuma mbele gurudumu la siasa zake za kupenda kujitanua na inapokuwa na uwezo huwa haisiti kuanzisha vita. Hatua ya utawala ghasibu wa Israel ya kuanzisha vita mara chungu nzima dhidi ya wananchi wa Palestina na mataifa mengine tangu ulipoasisiwa, ni ushahidi tosha wa kuthibitisha madai haya. Hii ni katika hali ambayo, baadhi ya wachambuzi wa mambo wameyatathmini matamshi hayo ya vitisho ya Israel kwamba, ni vita vya kisaokolojia vya utawala huo ghasibu. Kundi hilo la wajuzi wa mambo linaamini kwamba, hatua hiyo ya Israel ina lengo la kuzusha anga ya hofu na wasiwasi na hivyo kupata upendeleo inaotaka na wakati huo huo kuwasukuma Wapalestina upande wa duru nyingine ya mazungumzo eti ya mapatano. Aidha lengo jingine kwa mujibu wa weledi hao wa mambo ni kuvuruga hali ya mambo huko Palestina na hivyo kuzuia kufikiwa mwenendo wa maridhiano ya kitaifa. Ni kwa kuzingatia uhakika huo ndio maana baadhi ya wataalamu wa mambo wakasema kuwa, vitisho vipya vya Israel vina maslahi ya ndani tu.Hapana shaka kuwa, kushadidi matatizo ya kiuchumi, kuongezeka malalamiko ya ndani na vilevile kushika kasi mivutano ya kisiasa ndani ya utawala huo bandia katika miezi ya hivi karibuni ni mambo ambayo yamewafanya viongozi wa Tel Aviv wafanye kila wawezalo kuzipotosha fikra za waliowengi ulimwenguni kuhusiana na hali halisi ya mambo huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.Ukweli wa mambo ni kuwa, ili kukabiliana na utawala huo ambao miamala yake haijasimama juu ya mantiki na akili inapasa kudumisha muqawama na mapambano jambo ambalo daima limekuwa likifanywa na wananchi madhulumu wa Palestina.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA