Watu 20 wamebainika kuuawa katika hujuma ya kundi la kigaidi la Al Shabab mjini Mogadishi.Maafisa wa usalama wanasema watu 20 walipoteza maisha katika hujuma ya Ijumaa usiku ya magaidi wa Al Shabab wanaofungamana na mtandao wa Al Qaeda, dhidi ya Hoteli ya Somali Youth League.Magaidi wakufurishaji wa Al Sahaba Alhamisi iliyopita pia walishambulia eneo moja karibu na Ikulu ya Rais wa Somalia ambapo watu wanne waliuawa na wengine 8 kujeruhiwa.Hivi karibuni mjumbe maalumu wa Umoja wa Afrika nchini Somalia ametahadharisha kuhusiana na harakati za kundi la kigaidi la al-Shabab.Francisco Madeira ametoa indhari hiyo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Mogadishu Somalia na kutangaza kuwa, wanachama wa al-Shabab wana mpango wa kuvichafulia jina vikosi vya kusimamia amani vya Umoja wa Afrika nchini humo AMISOM.