SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 27 Februari 2016

T media news

Aal Khalifa washindwa kuzuia Sala ya Ijumaa Bahrain

Hatua za askari polisi wa utawala wa Aal Khalifa za kutaka kuwazuia wananchi wa Bahrain wasishiriki kwenye Sala ya Ijumaa zimegonga mwamba.Askari hao walishindwa kuwazuia waumini kushiriki kwenye Sala hiyo ambayo ilisaliwa kwa wito uliotolewa na maulamaa wa nchi hiyo.Katika kuendeleza sera za ukandamizaji za utawala wa Aal Khalifa, askari polisi wa utawala huo jana asubuhi walizifunga njia zote zinazoelekea eneo la Addaraz mahala alikozaliwa Sheik Ali Salman, Katibu Mkuu wa harakati ya Kiislamu ya Al-Wifaq ili kuzuia kusaliwa Sala ya Ijumaa katika eneo hilo.Hata hivyo bila kujali hatua za askari hao, wananchi wa Bahrain walisali sala hiyo katika barabara za kandokando ya msikiti wa Imam Sadiq (AS) katika eneo la Addaraz huko magharibi mwa mji mkuu Manama, sala ambayo iliyosalishwa na Allamah Sheikh Muhammad Sanqur.Tangu mwaka 2011 hadi sasa, Bahrain imekuwa uwanja wa malalamiko ya wananchi dhidi ya siasa za utawala wa kidikteta wa Aal Khalifa. Mauaji, ukandamizaji na utiaji nguvuni watu yamekuwa ndio maelekezo makuu yanayotekelezwa muda wote na vikosi vya polisi ya utawala huo wa kifamilia.../