SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 27 Februari 2016

T media news

Boko Haram 92 waangamizwa nchini Cameroon

Jeshi la Cameroon limetangaza kuwa, limefanikiwa kuwauwa zaidi ya wanachama 90 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram.Duru za habari zinaripoti kutoka Yaounde mji mkuu wa Cameroon kwamba, jeshi la nchi hiyo limefanya operesheni kali ya kijeshi dhidi ya kundi la Boko Haram na kuwaua wapingaji 92 wa kundi hilo. Issa Tchiroma Bakary, Waziri wa Mawasiliano wa Cameroon amesema kuwa, operesheni ya jeshi la nchi hiyo ilitekelezwa katika kijiji cha Kumshe cha Nigeria kilichoko katika mpaka wa nchi hiyo na Cameroon. Amesema kuwa, wanajeshi wawili wa Cameroon wameuawa katika operesheni hiyo. Aidha taarifa zaidi zinasema kuwa, wakazi 850 wa kijiji cha Kumshe cha Nigeria wamefanikiwa kuokolewa katika operesheni hiyo ya kijeshi.Zaidi ya watu 1,200 wameuawa katika hujuma za Boko Haram nchini Cameroon tangu lililopoanzisha mashambulizi yake dhidi ya nchi hiyo mwaka 2013.Kundi la Boko Haram limepanua mashambulizi yake kutoka Nigeria hadi katika nchi jirani za Chad, Cameroon na Niger. Inadaiwa kuwa kuna wanamgambo 8700 wa Boko Haram kwenye eneo hilo.Hivi karibuni Waislamu na Wakristo wa Cameroon walipendekeza mpango mpya wa kukabiliana na mashambulio ya kundi la kigaidi la Boko Haram. Mpango huo ambao unaungwa mkono na viongozi wa serikali, unalenga kulinda misikiti na makanisa mkabala na mashambulio ya Boko Haram.