Staa wa muziki Ali Kiba amesema harakati zake za muziki zilianzia kwenye muziki wa Hip Hop.
Staa wa muziki Ali Kiba Muimbaji huyo ambaye ameachia video ya wimbo Lupela wiki chache zilizopita, ameiambia Chill na Sky kuwa wakati huo kila msanii alikuwa anarap.
“Wakati nipo shule ya sekondari huko Mwanga, nilikutana na wasanii wa Hip Hop wanachana tu, hata mimi kipindi hicho nilikuwa nachana pia, muziki ambao ulikuwa umeanza ni wakuchana,’ alisema Kiba.
Aliongeza, “Kwa hiyo na mimi nilikuwa kati ya wale walioanza, malegendary, akina Professor Jay, akina AY, Sugu na watu wengine. Nilikuwa nikiwasikiliza sana, kwa hiyo nikapata nafasi ya kuadapt vitu, nikaanza kujifunza kidogo kidogo kwa sababu muziki ulikuwa ndani yangu lakini watu walikuwa hawajui. Kwa hiyo nilichokuwa nakifanya nilikuwa wanaentertain wenzangu kwa kurap kidogo,” alisema Ali Kiba.
Pia Ali Kiba alisema wakati huo alikuwa hatumii jina Ali Kiba, kwani alikuwa anaitwa Dogo Ali. harakati zake za muziki zilianzia kwenye muziki wa Hip Hop.