Ameanga dunia Mwongozaji filamu (director) aliyetengeneza filamu za Kisa cha As-habul Kahf na Kisa cha Maisha ya Nabii Yusuf (as) ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 63.
انا لله وانا اليه راجعون
Farajullah Salahshur, mwongozaji filamu (director)maarufu wa Kiirani aliyetengeneza filamu za Kisa cha As-habul Kahf na Kisa cha Maisha ya Nabii Yusuf (as) ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 63. Allah amrehemu, amlaze mahala pema peponi na amfufue pamoja na Mitume wake watukufu, amin.
Salahshur alikuwa tayari amesha andika pia kisa cha filamu ya Maisha ya Nabii Musa AS; na uchukuaji filamu wake ulikuwa uanze miezi michache iliyopita lakini mauti hayakumpa fursa ya kukamilisha kazi hiyo ya kheri. Inshaa Allah Mola amlipe thawabu ya amali hiyo tukufu kwa nia yake, amin.