SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 28 Aprili 2016

T media news

BAYERN YATULIZWA VICENTE CALDERON


Goli pekee la Saul Niguez limeiweka Atletico Madrid kwenye nafasi nzuri ya nusu fainali ya Champions League dhidi ya miamba ya soka la Ujerumani Bayern Munich.

Niguez akiipangua ngome ya ulinzi ya Bayern kabla ya kuukunja mpira kwenye kona ya goli na kuipa timu yake ushindi mwembamba wa mechi ya kwanza kabla ya kurudiana kwenye game ya pili itakayopigwa Ujerumani.

Bayern walitawala kipindi chote cha pili, shuti la David Alaba akiwa umbali wa mita 35 liligonga post ya juu ya lango la Atletico kabla ya golikipa wa Atletico kufanya kazi ya ziada kuokoa shuti jingine la Arturo Vidal.

Atletico walifanya shambulizi la kushtukiza (counter attack) lakini shuti la Torres liligonga mwamba.

Timu hizo zitakutana tena kwenye mchezo wa marudiano kwenye dimba la  Allianz Arena Jumatano ya juma lijalo kuamua nani atakutana na Manchester City au Real Madrid kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa May 28.

Takwimu muhimu

Atletico wameshinda michezo 13 kati ya michezo 17 ya Champions League kwenye uwanja wao wa nyumbani wakiwa chini ya Diego Simeone, wakitoka sare mara mbili na kupoteza mchezo mmoja.Atletico wamezifunga timu 23 kati ya 25 ambazo wamekutana nazo msimu huu kwenye mashindano yote waliyocheza, timu pekee walizoshindwa kuzifunga ni Villarreal na PSV Eindhoven.Bayern Munich hawajashinda kwenye michezo yao nane iliyopita ya Champions League waliyocheza ugenini kwenye hatua ya mtoano, wametoka sare mara nne na kupoteza michezo minne.Robert Lewandowski ameshindwa kufunga goli katika michezo nane iliyopita ya Champions League akiwa nje ya Allianz Arena.Mlinzi wa Bayern David Alaba amecheza mchezo wa 50 kwenye michuano ya Champions league ikiwa ni michezo mingi zaidi ya mchezaji yeyote wa Austria.