SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 11 Machi 2016

T media news

KILIMO BORA CHA ALIZETI


Alizeti ni kati ya mazao yanayotoa mbegu za mafuta. Hutoa mafuta kati ya asilimia 45-55 na mashudu yake ni chalula cha mifugo. Alizeti huvumilia ukame na hulimwa kwa ajili ya biashara na matumizi ya nyumbani. Wakulima huvuna kiasi kidogo, kati ya gunia 3-5 kwa ekari. Hivyo kwa mavuno mengi na bora, mkulima anashauriwa kuzingatia mambo yafuatayo:-

1. KUANDAA SHAMBA.
Unashauriwa kutayarisha shamba lako mapema kwa kukatua ardhi na kulainisha vizuri. Samadi yaweza kuchanganywa vizuri na udongo wakati wa kuandaa shamba.

2. WAKATI WA KUPANDA.
Maeneo yenye mvua nyingi alizeti huanza kupandwa mwishoni mwa mwezi Januari mpaka katikati ya mwezi Februari. Maeneo yenye mvua kidogo alizeti hupandwa mwezi Desemba hadi Januari.

3. KIASI CHA MBEGU NA UPANDAJI.
Kiasi cha kilo 3-4 za mbegu zinatosha kupanda eneo la ekari moja. Panda mbegu 3-4 ktk kila shimo kwa nafasi ya sentimita 75 kutoka mstari hadi mstari na sentimita 30 kutoka shimo hadi shimo. Shimo la mbegu liwe na kina cha sentimita 2.5-5. Wiki mbili baada ya kuota, punguza miche katika kila shimo na kubakiza mche mmoja.

4. KIASI CHA MBOLEA.
Mbolea zinazofaa kwa kilimo cha alizeti ni zile za kupandia na kukuzia hasa kwenye maeneo yasiyo na rutuba. Wakati wa kupanda tumia nusu mfuko kwa ekari moja ya mbole ya kupandia na mfuko mmoja kwa ekari moja ya mbolea ya kukuzia kwa kuigawa mbolea hiyo mara mbili. Nusu ya kwanza iwekwe wakati wa kupanda na nusu ya pili iwekwe wiki mbili baadaye.

5. PALIZI.
Alizeti hukua taratibu ktk wiki za mwanzo. Hivyo unashauriwa kupalilia mapema kupunguza hasara. Katika maeneo yaliyo na magugu machache, palizi moja tu inatosha. Vile vile maeneo yenye upepo mkali, wakati wa kupalilia inulia matuta kuzuia kuanguka.

6. FUNZA WA VITUMBA(American bollworm).
Funza huyu hutoboa mbegu changa kuanzia mara tu vitumba vya maua vikifunguka mpaka karibu na kukomaa kwa mbegu.

Tumia dawa yoyote ya kuulia wadudu.