SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 6 Machi 2016

T media news

VITAMINI C NA NGOZI YENYE AFYA


Vitamini C(ascorbic acid) ni miongoni mwa kundi la vitamini zinazochanganyika na maji(B na C). Uwezo wa kuondoa sumu (antoxidants) wa vitamini C na usaidizi wake katika kutengeneza kollageni, huifanya vitamini hii kuwa muhimu kwa afya ya ngozi. Tafiti zinaonyesha kuwa matumizi ya vyakula vyenye vitamini hii, ni yenye faida kwa seli za ngozi, na tafiti hizi pia zimeonyesha kuwa vitamini C husaidia kuzuia madhara ya mionzi hatari kutokana na miale ya jua (U.V radiation) na pia kusaidia kupona kwa haraka ngozi iliyoathirika na mionzi hiyo hata pia maambukizi ya
vijimelea.
Matumizi makubwa ya vyakula vyenye Vitamini C yamekuwa yakihusishwa na kupungua kwa hatari ya kuwa na ngozi iliyo kavu na iliyokunjamana, na hii inadhihirisha kuwa Vitamini C huzuia upotevu wa maji kutoka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuwa nyororo.
Ni muhimu na kujitahidi mlo wako kuwa na vitamini C ya kutosha kutokana na umuhimu wake kwa ngozi yako. Uwezo wa vitamini C kuondoa sumu pamoja na kusaidia utengenezaji wa kollageni husaidia ngozi yako kutokuwa ngumu na isiyokunjamana.
Mbali ya faida kwa ngozi, kihistoria vitamini C ilitumika na hutumika kutibu ugonjwa uijulikanao kama scurvy. Scurvy ni ugonjwa ambao dalili zake ni kuwa na vidonda mdomoni,uambukizi katika fizi ambao huambatana na kutoka damu katika fizi. Ugonjwa huu ni nadra siku hizi kutokana na ongezeko la matumizi ya vyakula vyenye vitamini C, lakini ni tatizo linalowakumba zaidi mabaharia na maharamia wanaosafiri baharini kwa miezi kadhaa, na hii ni hutokana na upungufu wa vyakula vyenye vitamini C.
Siku hizi Vitamini C hutumika kuzuia na kutibu homa ya mafua,fizi kutoa damu, chunusi, uambukizi katika ngozi, kifua, kuimarisha kinga ya mwili, kusaidia kupona kwa vidonda vya tumbo pia husaidia kupona kwa uambukizi wa kibofu na tezi dume.
Matumizi mengine ya vitamini C ni pamoja na kusaidia kusharabiwa kwa madini ya chuma kwa wagonjwa wenye upungufu(anemia) wa madini haya.
Vyakula vyenye vitamini hii kwa wingi ni matunda na mbogamboga.Vyakula hivi ni kama machungwa, zabibu, nanasi,embe,pilipili, limao,viazi vitamu na mboga za majani.