SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 18 Aprili 2016

T media news

SIMBA INAJIFUNGA YENYEWE

Unaweza kusema Simba ni kama imejifunga yenyewe kwenye mchezo wake wa ligi wa Jumapili dhidi ya Toto Africans ya Mwanza au kwa maneno ya vijana wa mjini wanasema ‘wamejilipua’ wenyewe kwa mabomu yao.

Katika kikosi cha Toto Africans kilichoichapa Simba 1-0, kiliundwa na wachezaji vijana wa walionunuliwa na Toto kutoka Simba. Wachezaji hao ni Carlos, Chuku, Hassan Hatib ambao wote walicheza kwenye aneo la ulinzi, Seseme alicheza kama kiungo wa kati wakati Edward Christopher alicheza kama mshambuliaji.

Kwenye benchi alikuwepo Japhet wakati wachezaji wengine ambao hawakuwepo kwenye plan ya mechi hiyo  ni Miraji Madenge na Ahmad Waziri ‘Kuku’.

Ilikuwa ni lazima Simba wafungwe kutokana na kocha wa wa Toto John Tegete kuwaamini vijana watano aliowachukuwa kutoka Msimbazi na kuwaambia kuwapa majukumu ya kudhihirisha kwamba, wao ni bora na walistahili kukitumikia kikosi cha kwanza cha Simba kutokana na uwezo mkubwa waliokuwa nao.

Klabu ya Simba imepoteza hazina kubwa ya vina wake wengi ambao ilitumiagharama na muda mwingi kuwaandaa lakini leo imebakiwa na wachache kati ya hao huku ikiwa imesheheni wachezaji wengi wa kigeni inaowalipa mishahara mikubwa ukilinganisha na uwezo wao uwanjani.

Ramadhani Singano na Ibrahimu Twaha ni nyota wengine ambao waliikacha Simba licha ya kuwa na viwango vya juu na sasa wanatamba kwenye timu nyingine na kuwatesa kila wanapokutana kwenye michezo ya ligi.

Kwenye mchezo kati ya Simba dhidi ya Toto unaweza kusema Simba ilijifunga yenyewe kwasababu kwa asilimia nyingi timu ya Toto ilijengwa na wachezaji wa Simba.

John Tegete alikataa timu yake kuitwa watoto wa Yanga na akahoji kwanini timu yake haiitwi watoto wa Simba kwasababu kikosi chake cha kwanza kilikuwa na vijana watano kutoka Simba.

Mimi nimechukuwa wachezaji watano kutoka Simba nimewapeleka Mwanza na leo (jana) wote wamecheza, unasemaje sisi ni watoto wa Yanga? Hayo ni mawazo potofu kwasababu timu yetu inavaa jezi zinazofanana na zile za Yanga”, alilalama Tegete.