Mamilioni ya ndege wahamiaji wameonekana juu ya Israel, na kusababisha usumbufu mkubwa kwa usafiri wa anga wa kijeshi na mifumo ya rada.



Ndege hao, wa spishi tatu tofauti, wanajitokeza kama ndege za adui kwenye mifumo ya rada, ingawa kwa macho ni makundi ya ndege.

Ndege hao, ikiwa ni pamoja na Mbayuwayu, Tai na kiruka njia wameonekana kwenye Hula Lake Park kaskazini mwa Israel.

Uhamaji huu mkubwa wa ndegehai unatokea wakati wa mvutano mkubwa kati ya Israel na Iran, na kusababisha changamoto kwa operesheni za kijeshi na usalama wa anga.

Chombo cha habari cha Middle East Eye (MEE) kimeripoti mnamo Machi 13, 2026, kuwa Jeshi la Anga la Israel lina wasiwasi na dhidi ya ndege hao wanaovuka anga la Israel wakati wa msimu wa uhamiaji.

Ripoti hiyo ilieleza kuwa, ndege hao huonekana kwenye rada kama "vitu vinavyotia shaka" au ndege vamizi na wakati mwingine huonekana kama ndege zisizo na rubani (drones).

Jarida la Digivestasi lilimnukuu mtaalamu wa ndegehai Yaron Charka mnamo Machi 13, 2026, akisema kuwa uhamiaji wa ndege hao unaonekana kuruka katika kimo sawa na ndege za kivita, hali inayoongeza hatari ya migongano na kutatanisha ulinzi wa anga.

Jarida la Aurora Israel liIlichapisha taarifa kuhusu changamoto ya operesheni za anga kutokana na mkusanyiko mkubwa wa ndege ikitaja ndege aina ya Mwari, Korongo na Kurungu ambao rada hutambua kama vitu visivyojulikana (unidentified flying object)