Marekani imefanya shambulizi katika miundo mbinu kisiwani Kharg,
Marekani imefanya shambulizi katika miundo mbinu kisiwani Kharg, lakini pamoja na kupiga miundombinu mingine kwenye kisiwa hiki operation hii haikugusa kabisa moyo wa Iran, kitovu cha mafuta cha Iran ambacho ni Kharg Oil Hub.
Sasa baada ya tukio hili la mashambulizi vyombo vya habari vya serikali ya Iran viliripoti kuwa hakukuwa na uharibifu wa miundombinu ya mafuta kwenye kitovu cha Kisiwa cha Kharg, lakini katika taarifa Iran imeonya vikali kuhusu matokeo ya “shambulio lolote” kwenye kitovu cha miundombinu yake ya nishati. Imemkanya Marekani kuto thubutu kabisaa kugusa Kharg Oil Hub.
Kisiwa cha Kharg, kisiwa kidogo lakini cha kimkakati kilicho maili 15 kutoka pwani ya Iran katika Ghuba ya Uajemi, ni nyumbani kwa kituo cha mafuta ambacho husafirisha 90% ya mauzo ya mafuta ya nchi hiyo. Pia kuna uwezo wa kijeshi huko, ikiwa ni pamoja na ulinzi wa anga na migodi iliyozikwa chini ya ardhi.
Katika kujibu hili Iran imesema “Iwapo hili litatokea, miundombinu yote ya mafuta na gesi katika eneo ambalo Marekani na washirika wake wana maslahi itachomwa moto na kuharibiwa vibya na Makombora ya Iran,” vikosi vya kijeshi vya Iran vilisema.
Kisiwa cha Kharg ndicho “mhimili” wa miundombinu ya biashara ya mafuta ya Iran, kulingana ripoti za uchambuzi, Iran ilipata dola bilioni 53 za Kimarekani katika mapato ya mauzo ya nje ya mafuta mwaka 2025, karibu 11% ya Pato la Taifa la kila mwaka.

Maoni
Chapisha Maoni