Tamko la Brigedia Jenerali Ali Fadavi (IRGC):
"Kama adui angeshinda vita hivi, wasingehitaji ulimwengu mzima uingilie kati kupatanisha na kutangaza usitishaji vita.
Tuna makombora yanayorushwa kutokea chini ya maji kwa kasi ya mita 100 kwa sekunde, na hakuna yeyote duniani mwenye teknolojia hii isipokuwa sisi na Urusi; na huenda tukayatumia katika siku zijazo.
Kama Wamarekani wangejua kiasi cha kodi zao kinachotumika kujenga kambi za kijeshi Mashariki ya Kati, wangeandamana na kupindua serikali yao leo hii. Kwa sasa, hakuna meli yoyote ya kivita ya Marekani iliyo ndani ya umbali wa kilomita 700 kutoka nchini Iran.
Jeshi la Wanamaji la Marekani limekimbia kwa sababu linatambua kuwa tuna mpango maalumu wa kuzamisha meli zao kubwa za kubeba ndege za kivita (aircraft carriers). Aidha, tumetungua ndege ya kivita ya Marekani aina ya F-15 upande wa kusini mwa Tehran."
