Ewe ndugu yangu Muislamu,
Leo ni Ijumaa ya mwisho katika mwezi mtukufu wa Ramadan.
Ni siku ya tafakari, shukrani na kujikumbusha neema kubwa tuliyopewa.
Ramadhan imekuja na rehema zake, imetufundisha kuswali zaidi, kusoma Qur’an, kufanya dhikri na kujiepusha na maasi.
Sasa tunapokaribia mwisho wake,
jiulize nafsi yako:
🌿 Je, Ramadhan imebadilisha moyo wangu?
🌿 Je, nimekaribia zaidi na Allah?
🌿 Je, nitaendelea na ibada hata baada ya Ramadhan?
Ijumaa hii ya mwisho ni nafasi nyingine ya:
✨ Kutubu kwa dhati.
✨ Kuomba msamaha kwa Allah.
✨ Kuomba akubali ibada zetu zote.
Usiruhusu Ramadhan iondoke bila dua zako nyingi.
Kumbuka 🌿
Huenda hii ikawa Ramadhan ya mwisho katika maisha yetu,
na huenda tusipate tena nafasi ya kukutana nayo.
🤲 Dua
“Ewe Allah,tupokee funga zetu, swala zetu na dua zetu za Ramadhan.
Usifanye Ramadhan iwe shahidi dhidi yetu bali iwe shahidi kwa faida yetu.
Utujalie kufikia Ramadhan nyingine tukiwa katika afya na imani.Aamiin.”
#Uislamunidiniyahaki
#MwenyeziMungundiyeajuayezaidi
