Sunnah za Eid al-Fitr
✔ Kula kabla ya kwenda kuswali (hasa tende kwa idadi ya witri)
✔ Kuoga na kuvaa nguo nzuri
✔ Kupaka manukato (kwa wanaume)
✔ Kwenda kuswali uwanjani
✔ Kuleta Takbira kwa wingi
Imepokewa kutoka kwa Anas ibn Malik:
Mtume ﷺ hakuwa akienda kuswali Eid al-Fitr mpaka ale tende kwa idadi ya witri. (Sahih al-Bukhari)
🌿 Takbira za Eid
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar,
Laa ilaaha illa Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar,
Wa lillaahil hamd.
Allahu Akbar Kabiiraa,Walhamdulillahi Kathiiraa, Wasubhaanallahi Bukratan wa Asiilaa.
Laa ilaaha illa Allaahu, wa laa na‘budu illa iyyaahu, mukhlisiina lahud-diina walaw karihal-kaafiruun.
Laa ilaaha illa Allaahu wahdahu,sadaqa wa‘dahu,wa nasaha ‘abdahu, wa a‘azza jundahu,wa hazamal ahzaaba wahdah.
Laa ilaaha illa Allaahu,Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, wa lillaahil-hamd.
🌿 Yaliyo Sunnah Kufanya Siku ya Eid
• Kuoga na kuvaa vizuri
• Kupaka manukato
• Kuandaa chakula kizuri
• Kuwatembelea ndugu, marafiki na majirani
• Kuwasaidia maskini na mayatima
• Kupeana zawadi
• Kuonyesha furaha kwa halali
⚠️ Tahadhari Siku ya Eid
Muislamu anatakiwa ajiepushe na:
• Ulevi
• Muziki na mambo ya upuuzi
• Mchanganyiko usiofaa wa wanaume na wanawake
• Zinaa na maasi
Kwa sababu Eid ni:
👉 Siku ya kumshukuru Allah, si kumuasi.
.
.
.
#Uislamunidiniyahaki
#MwenyeziMungundiyeajuayezaidi

Maoni
Chapisha Maoni