Tutapitwa kila kitu na wa Tz . William Rutto.

 


Nashangaa kuona Media kubwa ya Kwetu kumilikiwa kirahisi na Mfanya biashara kutoka Tanzania, japo sio maswala ya kubagua watu wa njee kuja kuwekeza nchini kwetu, Ila ki ukweli wakenya ni kama hatuna kauli mbele ya jirani yetu, kwahiyo jitahidini wakenya kuwekeza na nyie hata #Tanzania maana tusipo kuwa makini tutapitwa kila kitu na wa Tz . William Rutto.


Hii ni baada ya Mfanya biashara kutoka Tanzania Rostam,kununua hisa nyingi katika kampuni ya, Standard Group PLC ya nchini Kenya.


*Hapa kuna mambo muhimu unayopaswa kufahamu kuhusu hatua hi:*

#Rostam Aziz: Ni mwekezaji na mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania (miliki wa makampuni kama Taifa Gas). Nchini Tanzania, anamiliki kampuni ya New Habari (2006) Ltd, inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Rai, na Bingwa. Standard Group PLC: Hii ni moja ya kampuni kongwe na kubwa zaidi za habari nchini Kenya. Inamiliki vituo maarufu kama KTN Home, KTN News, gazeti la The Standard, na vituo vya redio kama Radio Maisha. 2. Sababu za Mauzo Standard Group imekuwa ikipitia changamoto kubwa za kifedha kwa miaka kadhaa sasa, ikichangiwa na:

Kupungua kwa mapato ya matangazo. Mabadiliko ya teknolojia (watu wengi kuelekea kidijitali). Madeni makubwa yanayoikabili kampuni hiyo.