Hii siyo scene kutoka kwenye filamu ya Interstellar bali ni uhalisia wa sasa! Watu takriban 500 duniani kote kwa sasa wamehifadhiwa kwenye mitungi mikubwa ya nitrogen ya maji (Dewars) kufuatia kifo chao cha kitabibu.
Inafanyaje kazi?
Badala ya kuzikwa au kuchomwa, miili hupitia mchakato unaitwa Vitrification. Maji ya mwilini huondolewa na kuwekwa kemikali maalum zinazozuia barafu isitengenezwe na kuharibu seli, kisha wanahifadhiwa kwenye baridi kali ya -196°C.
Moja ya watu waliomo kwenye mitungi hii ni pamoja na bilionea wa Bitcoin Hal Finney na gwiji wa baseball Ted Williams wengi wao wametumia bima zao za maisha (Life Insurance) kugharamia utaratibu huu wa bei mbaya
Lengo la watu hawa kuwekwa kwenye mitungi hii ni wanasubiri "Future Tech." ambayo kwa maendeleo ya Artificial Intelligence (AI), Nanotechnology na dawa za kisasa katika karne zijazo zitaweza kurekebisha miili yao na kuwarudishia uhai.
Je, ungependa kugandishwa uje kuona dunia itakuwaje baada ya miaka 150 au unadhani "Kifo ni Kifo tu?
