Qur'an ni muongozo ulioshuka kwa wanadamu ili kuyaongoza maisha ya mwanadamu na ni uthibitisho kwa wale ambao walikuwa na shaka juu ya jambo fulani. Unajua nini Allah SW alisema kwa Nabii wake kwa wale ambao wanabisha juu ya maneno ya Allah? Alimwambia
Q(18:22) Basi usibishane juu yao ila kwa mabishano ya juu juu tu hivi.
Kwa watu wa zama zile walikuwa wagumu sana kuelewa jambo la KUFUFULIWA BAADA YA KUFA KWETU, walikuwa wakijiuliza 'je baada ya kufa kwetu kuna kufufuliwa?' Basi Allah SW aliwajibu kwa kuwapa ushahidi wa dalili nyingi zaidi na hapa tunakupa dalili TATU ambazo Allah SW aliwapa kupitia watu waliolala Miaka mingi zaidi na muujiza wake kwa Nabii Ibrahim AS.
1- WATU WA PAMGONI
Katika Surah ya 18 kwa jina la Al Kahf sura ambayo ina fadhila nzuri kwa muislamu anayesoma siku ya Ijumaa aya kumi za mwanzo au za Mwisho basi hupata Nuru Ijumaa mbili, na pia ni surah inayotajwa ikisomwa itamlinda mja na masihi dajjal (Masihi wa Uwongo)
Katika Surah hii Allah SW anatupatia kisa cha watu wa pangoni ambao katika Qur'an hawakutajwa kwa idadi yao kamili, walikuwa ni watu wacha Mungu sana waliomtegemea na Kumuabudu Allah pekee katika nyakati ambazo walitakiwa kuabudu masanamu na ilikuwa ni siri miongoni mwao kumuabudu Allah, hivyo siku moja siri yao waliitoa kwa kushuhudia mbele za watu kwamba MOLA WAO NI ALLAH, kwa mujibu wa Qur'an watu hawa walifanikiwa kwenda katika moja ya pango na kujificha huko na mwisho walipatwa na usingizi na wakalala wakiwa wao na Mbwa mmoja, Baadhi ya watafsiri wana walilala humo miaka 360 na miongoni mwa watafsiri wanasema ni 309 na wengine wanasema ni 300. Ni kisa ambacho kinapatikana katika Surah ya 18 kuanzia Aya ya 9 hadi ya 26 unaweza funua Qur'an kusoma zaidi na kimeelezewa kwa ufupi zaidi
2- KISA CHA NABII IBRAHIM
Je unafahamu kwamba kuna dalili ambayo Allah SW alimwambia Nabii Ibrahim AS, kufuga ndege Wanne kisha awachinje na kila kipande aweke juu ya Mlima tofauti iliyo mbalimbali na kisha awaite hao ndege , na alipowaita waliamka na kuja mbiombio, Unaweza soma zaidi katika Qur'an Surah ya Al Baqarah sura ya Pili (2) katika Qur'an, kuanzia Aya ya 260.
3- KISA CHA UZEIR
katika surah ya pili (2) Al Baqarah Allah katuelezea jinsi shaka la Uzeir kwa kufufuliwa watu alijiuliza "Ataufufuaje Mwenyezi Mungu mji huu baada ya kufa kwake?" Basi Allah akamfisha kwa mtu huyu kulala mahali pale yeye na mnyama wake kwa muda wa miaka 100, Unaweza kusoma zaidi katika Surah ya Al Baqarah aya ya 259. Funua Qur'an kusoma zaidi.
naipenda_qur_an
