Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV, amerejea kutoa wito wa kusitishwa kwa vita



 Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV, amerejea kutoa wito wa kusitishwa kwa vita katika Mashariki ya Kati na kufunguliwa tena kwa njia za mazungumzo. Amesema kuwa kwa zaidi ya wiki mbili, watu wa eneo hilo wameendelea kupitia ukatili mkubwa wa vita, hali iliyosababisha vifo vya maelfu ya raia na kuwalazimisha wengine wengi kuyakimbia makazi yao.


Papa aliwatakia faraja wale waliopoteza wapendwa wao kutokana na mashambulizi yaliyolenga maeneo ya huduma za jamii kama shule, hospitali na makazi. Aidha, ameonyesha wasiwasi wake kuhusu hali ya Lebanon, akisisitiza kuwa hali ya nchi hiyo inahitaji umakini maalum.

Katika wito wake, amehimiza wahusika wa mgogoro huo kusitisha mapigano na kurejea kwenye njia ya mazungumzo, akionya kwamba vurugu haziwezi kuleta haki, utulivu wala amani inayosubiriwa na watu wa eneo hilo.