Kati ya Iran na Israel ni Taifa Lipi Limekuwa Tishio la "Kigaidi" Ulimwenguni? Tuangalie Hoja za Kisayansi Zifuatazo:
1. Uwazi na Mikataba ya Kimataifa - Tofauti kubwa kati ya mataifa haya mawili ipo kwenye ushirikiano wao na jumuiya ya kimataifa:
Iran na NPT: Iran ni mwanachama wa mkataba wa kuzuia uenezaji wa silaha za nyuklia (Non-Proliferation Treaty - NPT). Hii inaifanya Iran kuwajibika kisheria kuruhusu wakaguzi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) kukagua vituo vyake mara kwa mara. Ripoti nyingi za IAEA zimekuwa zikithibitisha kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kugeuza nyenzo za nyuklia kwenda kwenye matumizi ya kijeshi.
Israel na Usiri: Israel haijawahi kusaini mkataba wa NPT. Inafuata sera ya "Nuclear Ambiguity" (kutoweka wazi kama inazo au haina). Kutokana na kutosaini mkataba huo, Israel hailazimiki kuruhusu ukaguzi wa IAEA, jambo linaloifanya kuwa na "Ghala la Siri" ambalo halidhibitiwi na sheria za kimataifa.
2. Mafundisho ya Kidini na Kisiasa (Fatwa) - Iran imekuwa ikisisitiza kuwa mpango wake ni wa nishati ya kiraia na matibabu: Fatwa ya Kiongozi Ayatollah Ali Khamenei aliyetoa tamko rasmi la kidini (Fatwa) inayopiga marufuku utengenezaji na matumizi ya silaha za nyuklia, akizitaja kuwa ni "haramu" na kinyume na maadili ya Kiislamu. Hii ni nguzo muhimu ya kidiplomasia ambayo Iran huitumia kuonesha nia yake ya amani.
3. Historia ya Uvamizi na Uchokozi - Ili kupima "kitisho," ni muhimu kuangalia jinsi nchi inavyotumia nguvu zake za kijeshi. Rekodi ya Iran katika karne za hivi karibuni haijawahi kuanzisha vita au kuvamia nchi nyingine (Aggressive War). Operesheni zake nyingi zimekuwa za "kujihami" au kuunga mkono washirika wake ndani ya mipaka ya kikanda.
Rekodi ya Israel - Israel imehusika katika migogoro mingi ya kijeshi na uvamizi wa nchi jirani (kama Lebanon na maeneo ya Palestina). Kwa mtazamo wa kawaida tu, nchi yenye silaha za nyuklia ambazo hazijatambuliwa rasmi na ambayo ina historia ya mashambulizi ya kushtukiza inachukuliwa kuwa kitisho kikubwa zaidi kwa utulivu wa kikanda.
4. Makubaliano ya JCPOA
Iran ilionyesha utayari wa kupunguza uwezo wake wa kuratibu madini ya urani kwa kusaini makubaliano ya JCPOA (2015) na mataifa makubwa duniani. Hatua hii ya kukubali vikwazo na ukomo wa kiteknolojia ni ishara ya kufuata taratibu za kidiplomasia, tofauti na Israel ambayo haiko chini ya shinikizo lolote la kisheria la kupunguza uwezo wake.
Kitaalamu, Iran inaonekana siyo kitisho cha nyuklia kwa sababu imewekwa chini ya mifumo ya uangalizi (safeguards) ya kimataifa, wakati Israel inabaki kuwa kitisho kutokana na kutokuwepo kwa uwazi na kutofungwa na sheria yoyote ya kimataifa kuhusu silaha hizo. Kwa bahati mbaya, Ushoga wa Marekani na Israel umeendelea kuiharibu amani ya dunia kwa kuvamia nchi zilizokuwa zimetulia zikifanya mambo yao kivyao.
