Hadi sasa Charles Burton amebakiwa na siku moja tu ya kuishi. Ingawa ametumia zaidi ya miongo mitatu kwenye gereza la hukumu ya kifo (death row).
Burton, anayejulikana kama “Sonny” kwa familia na marafiki zake, amepangwa kunyongwa siku ya Alhamisi.
Taarifa kutoka CNN inasema Mzee huyo mwenye umri wa miaka 75, ambaye sasa anatumia kiti cha magurudumu, yuko kwenye hukumu ya kifo kwa kosa la mauaji ya Douglas Battle, licha ya ukweli kwamba yeye mwenyewe hakufanya tukio la kumpiga risasi lililosababisha kifo hicho.
“Sikumua mtu yeyote, hilo ni kweli, lakini nilifanya kosa kwa kuwa sehemu ya uhalifu huo,” Burton aliiambia CNN katika mahojiano.
“Nilifanya kosa, na inaonekana marafiki zangu wengi wamenisamehe. Natumaini hata nikinyongwa Alhamisi marafiki zangu watakumbuka kuwa nilikuwa rafiki wa kweli, rafiki mzuri.”
Alisema Burton.
Sasa hali ilikuwaje hadi kuhukumiwa kifo Ilihali anakiri kuto kuhusika katika mauaji?
Twende tuitazame hadithi yenyewe .
Mnamo Agosti 1991, Burton pamoja na Derrick DeBruce waliiba katika duka la AutoZone mjini Talladega.
Wakati walipovamia duka kwa lengo la kuiba, wateja kadhaa walikuwa wakipata huduma katika duka hilo. Na ndipo Derrick ambaye alikuwa rafiki wa Burton alimfyatulia risasi na kumuua mteja mmoja katika Duka Hilo.
Wote walifikishwa mahakamani na kusomewa hukumu ya kifo ambapo hakukuwekwa tarehe Kamili ya wao kuuwawa.
Ingawa Burton hakuwa mtu aliyepiga risasi na hata hakuwa ndani ya duka wakati mauaji yalipotokea, alihukumiwa kwa kosa la mauaji ya jinai ya kiwango cha juu (capital felony murder) na kuhukumiwa kifo na jopo la majaji mwaka 1992.
Tangu hapo walikaa katika gereza la kesi la mauaji wakisubiri tarehe kamili ya kutekelezwa kwa hukumu hiyo. Hata hivyo Mwaka 2014 rafiki yake DerrickDebruce alifariki Kwa ugonjwa akiwa gerezani.
Tangu hapo Burton alibaki gerezani kusubiri hukumu juu ya mauaji ambayo si yeye alihusika kupiga risasi hukumu ambayo inatarajia kutekelezwa Alhamisi hii.
Maoni yako ni yapi katika hili? Je adhabu hii inapaswa kutekelezwa ama Selikali inapaswa Kutazama Kwa jicho jingine juu ya hukumu hii?.
