Kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita, vita kubwa (kama hii ya Iran) zinaamua nani atatawala uchumi wa Dunia. Mfano mzuri ni baada ya Vita ya Kwanza ya Dunia (WWI) na Vita ya Pili ya Dunia (WWII) ambapo ramani ya nguvu za kiuchumi ilibadilika kabisa. Tushuke chini pamoja;
2. Ujerumani alikuwa KIRANJA kabla ya WWI
Kabla ya Vita ya Kwanza ya Dunia, Ujerumani ilikuwa;
- injini kubwa ya viwanda Ulaya.
- kinara kwenye mitikasi ya Kemikali,
- chuma na teknolojia za viwanda.
Lakini alipokinukisha tu uchumi wake ulipoteana, na kulazimika kulipa fidia kubwa kupitia Mkataba wa Versailles (Treaty of Versailles).
3. Uingereza ilipoteza uongozi baada ya WWII;
Kabla ya Vita ya Pili ya Dunia, Uingereza ilikuwa kitovu cha mifumo ya kifedha duniani. Sarafu ya Pound ndiyo iliyotawala biashara ya kimataifa. Baada ya kujizamisha kwenye vita;
- Uchumi wake ukajifia,
- makoloni yakapata uhuru,
- na nguvu ya kifedha ikahamia Marekani.
4. Marekani akawa kiranja Mkuu mpya;
Baada ya WWII, Marekani ilitoka akiwa na nguvu kwenye viwanda, uchumi ukapanda, na nguvu kubwa ya kijeshi. Ndipo akaenda kujisimika kwenye mfumo mpya wa fedha kupitia makubaliano ya #Bretton Woods ambayo yaliifanya dola ya Marekani kuwa sarafu kuu ya dunia. Bretton Woods Accords ilifanya;
- zaidi ya nchi 44 kubadili sarafu zao kwenda kwenye Dollars.
- Dollar ikakita mizizi kwenye dhahabu
- Na kisha ikaenda kwenye mafuta.
5. Mfumo wa Petrodollar ukaifaidisha Marekani
Kuanzia miaka ya 1970, mafuta mengi duniani yalianza kuuzwa kwa dola ya Marekani. Hapa USA alikubaliana na Saudi Arabia;
- auze mafuta kwa Dollar
-Halafu USA amhakikishie usalama Saudi Arabia.
Hili ndo chimbuko la mfumo unaoitwa Petrodollar ambapo nchi nyingi zinahitaji dola kununua mafuta, hivyo Marekani akawa na nguvu kubwa ya kifedha duniani tunayoiona hii leo.
6. Kihistoria Vita vina gharama kubwa kwa Kiranja Mkuu;
Historia inaonyesha hata mataifa makubwa hupata shida wanapoingia vita nyingi. Mfano ni Vita ya Vietnam na Vita ya Afghanistan (2001–2021) ambazo ziligharimu Marekani trilioni za dola. Gharama hizi husababisha;
- deni la taifa
-mfumuko wa bei
-Changamoto Za Kiuchumi.
Twende sasa kwenye vita ya Iran dhidi ya Marekani na Israel;
7. Iran ilipokaa ni mtego kwa Dunia;
Kijiografia Iran ipo kwenye njia muhimu sana ya mafuta duniani inayoitwa Strait of Hormuz. Sehemu kubwa ya mafuta (20%) kwa Siku ya dunia hupita katika njia hii nyembamba ya bahari. Ikiwa njia hii itaendelea kufungwa basi;
- bei ya mafuta duniani itapanda
- Kisha uchumi wa dunia utayumba.
8. Hesabu Za Mchina;
China kwa sasa inapambana kupunguza utegemezi wa dola kwa kukuza biashara ya mafuta kwa kutumia sarafu yake ya yuan. Ikiwa nchi nyingi zitaanza kutumia yuan;
- mahitaji ya dola yanaweza kupungua
-mfumo wa Petrodollar unaweza kupoteana .
Kumbuka Iran kaweka wazi “Nunua mafuta kwa Yuan uwe salama, au nunua kwa dollar uchezee kichapo, Hormuz.
9. Hapa ndo Dunia inaweza kuwa kwenye sura mpya;
Badala ya kuwa na Kiranja Mkuu mmoja ambaye anaamua kufanya anachojisikia yeye, dunia inaweza kuwA #MULTIPOLAR WORLD” ambapo nguvu zinagawanyika kati ya;
-Marekani,
-China,
- EU
-Urusi n.k.
10. Lakini pia Meza inaweza kupinduka;
Historia inaonyesha jambo moja wazi: vita vikubwa vinaweza kubadilisha kabisa nani anatawala uchumi wa dunia. Kutoka;
-Ujerumani kabla ya WWI, hadi Uingereza kabla ya WWII,
-Kisha Marekani baada ya WWII kwa miaka zaidi ya 50 Sasa.
Mgogoro unaohusisha Iran unaweza kuwa sehemu ya mabadiliko mapya ya misuli za kiuchumi duniani.
ππ»Je China π¨π³ atatoboa? Vipi USA πΊπΈ atabaki ana mtazama tu? Tuwe na subira.

