USIACHE ASILI MAFANIKIO YAKO MIKONONI KWAKO!

 


Iliki & Pilipili Manga Ni miongoni mwa mazao ya Asili yana faida lukuki kama tiba ya kimwili na kiroho.Yanafungua vifungo.. Ndio maana ukifungua jioni mwezi wa ramadhani upate uji au chai ya pilpil manga au iliki inafungua vifungo na tiba ya mwili hata vidonda tumbo.


💥NGUVU ZA KIROHO

Kuvutia wateja na bahati katika eneo lako la biashara. Tumia iliki na pilipili manga ya unga kupigia deki na kupulizia ndani ya eneo lako la biashara yako kila siku kabla hujaanza kufanya biashara. Huondoa nguvu za giza kuleta nuru ya mwangaza wa mafanikio.


Pia unaweza kutumia iliki na pilipili manga ya unga siku ya jumatatu usiku wa 6 kumwaga unga wake ndani ya eneo lako la biashara na kusubiri baada ya lisaa limoja au zaidi ukafagia kwa kutoa njee na mabaki hayo ya iliki na pilipili manga uliyofagia ukayafukia njee mbele ya eneo lako la biashara.


💥MVUTO WA MAPENZI/BIASHARA

Kwa, kutumia iliki na pilipili manga ya punje. Unaweza kuvutia unavyohitaji kwa kuvichoma kwa pamoja kwa manuizi mfano kama unamdai mtu na hataki kulipa ilihali uwezo wa kulipa anao fanya hii. Au umekimbiwa na mke au mume kwa sababu ambazo ni dhaifu fanya hii


#ZINGATIA 

Sio umefanya ufisadi katika mahusiano yako kama kuchepuka umegundulika ukataka kutumia dawa hiyo hapana. Mimi nawaelekeza wale waliodhulumiwa haki zao zao wanaodhulumu wenzao.


💥HUONDOA UCHAWI NA MAJINI

Twanga pilipili manga na iliki kwa pamoja, una uchuje unywe maji yake.  Na uwe unaogea.

Mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kwa siku 7 mfululizo. 


💥TIBA YA MWILI

Kusaidia katika mmeng'enyo wa chakula, Twanga pilipili manga changanya na asali tumia kwa kula kijiko kimoja asubuhi na jioni kwa siku 7 mfululizo.


💥HUONGEZA NGUVU ZA KIUME

Kuongeza hamu ya tendo la ndoa

Twanga iliki, pilipili manga, tangawizi na karafuu changanya na asali ya nyuki wadogo.

Unywe kijiko kimoja asubuh na jioni kwa siku 14 mfululizo.


💥JINO LINAUMA 

Tumia Iliki kuweka au kutafuna katika jino linalouma.


💥HUONGEZA KUMBUKUMBU Kupenda kunywa chai ya iliki na pilipili manga kunaweza kukuongezea uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu. Ni vema kufanya hivi kwa asubuhi kabla ya kula chochote.