June 2025 kwenye ile "Operation Midnight Hummer" aliidanganya dunia kuwa ameangamiza miundombinu yote ya nuklia ya Iran, tena akadai itawachukua miaka 30 kuijenga tena. Tarehe 29 December 2025, akaidanganya dunia kuwa uongozi wa Iran imeanza kurutubisha kwa wingi madini ya nyuklia kiwango kinachofikia kilogramu 400 kwa zaidi ya asilimia 60%.
Hapo jiulize ile propaganda ya June 2025 aliyojitamba nayo vipi? Tarehe 01 March 2026 akasema amevunja uongozi wote wa Iran kwa kumuua Ayatollah Ali Khamenei, akasema atamaliza vita kwa kuisambaratisha uongozi wote wa juu wa Iran, na Wairan wachukue nchi.
Tarehe 4 March 2026, akasema ameangamiza miundombinu yote ya makombora ya masafa marefu na ngome zote za kijeshi za aridhini, Majina na Angani za Iran hivyo Iran imedhoofishwa sana.
Tarehe 3 2026, Trump alilisifia jeshi lake kuwa lenye nguvu kuwahi kushuhudiwa duniani, akasema ataimaliza vita hii kwa ufanisi ndani ya siku chache.
Tarehe 6 March akiwa anapokea maiti za askari walio uwawa huko mashariki ya kati, akaeleza kuwa "vita itachukua muda mrefu kutokana na mashambulizi ya makombora ya Wairan na drone zao kuwa za gharama nafuu, hivyo wajiandae kwa vita ya muda mrefu".
Tarehe 6 March 2026 jioni akiwa na baraza la usalama la Marekani, akaeleza kulalamika kwa nchi washirika kugoma kumpa msaada wa kuisaidia Marekani kupambana na Iran, kasahau kuwa tarehe 3, yani siku 3 nyuma alijigamba kuwa jeshi la Marekani ni jeshi lenye nguvu zaidi duniani na ataimaliza vita ndani ya siku chache kwa ufanisi.
Tarehe 8 March 2026 Marekani inasema Wairan ni vichaa, hata yeye awailewi, anaomba msaada Hispania nayo ikagoma, Uingereza ikagoma, Ukraine ikakubali kutoa drone zake, siku hiyo hiyo anailalamikia Urusi kutoa msaada wa taarifa za kijasusi kwa Iran ili Iran ifanye mashambulizi kwenye ngome na meli zake.
Tarehe 9 March 2026 Marekani inataka nchi za kiarabu ziingie kwenye vita dhidi ya Iran, anasema atazipa msaada wa fedha, anatumia mbinu hiyo kuwauzia waarabu vita alafu yeye ajitoe ili vita ibaki mashariki ya kati yeye awauzie waarabu siraha.
