HABARI SANAA NA MICHEZO

Jumanne, 10 Machi 2026

T media news

HUKUMU YA MTU ASIE SWALI NA ANAE FUNGA LAKINI HASWALI


 

🔸سئل العلامة العثيمين رحمه الله تعالى - كما في مجموع الفتاوى ( ج ١٢ / ١٠١ - ١٠٣ )

ﻋﻦ ﺭﺟﻞ ﻻ ﻳﺼﻠﻲ الصلاﺓ ﺇطلاﻗﺎ ﻣﻊ ﺇﻗﺮاﺭﻩ ﺑﻮﺟﻮﺑﻬﺎ ﻭﻳﺼﻮﻡ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﻟﻜﻨﻪ ﻻ ﻳﺼﻠﻲ ﻫﻞ ﻳﺤﻜﻢ ﺑﺈسلاﻣﻪ؟

Aliulizwa Mwanachuoni Uthaymiin Allah amrehemu, kama katika kitabu "Majumu'ul fataawa" (juzuu ya: 12 / 101 - 103)

Kuhusiana na mtu ambae haswali kabisa, ingawa anakiri uwajibu wa swala, na anafunga Ramadhani, lakini haswali. Je, anahukumiwa kuwa ni Muislamu?


🔹ﻓﺄﺟﺎﺏ ﺑﻘﻮﻟﻪ: 

"اﻟﺼﻼﺓ ﺃﻣﺮﻫﺎ ﻋﻈﻴﻢ ﻭﺷﺄﻧﻬﺎ ﻛﺒﻴﺮ، ﻭﻫﻲ ﺁﻛﺪ ﺃﺭﻛﺎﻥ اﻹسلاﻣ ﺑﻌﺪ اﻟﺸﻬﺎﺩﺗﻴﻦ ﺑﺈﺟﻤﺎﻉ ﺃﻫﻞ اﻟﻌﻠﻢ، ﻭﻭﺭﺩ اﻟﻮﻋﻴﺪ اﻟﺸﺪﻳﺪ ﻓﻲ ﺇﺿﺎﻋﺘﻬﺎ ﻓﻲ اﻟﻜﺘﺎﺏ ﻭاﻟﺴﻨﺔ، ﻭﻻ ﺃﻇﻦ ﺃﻥ ﺃﺣﺪا ﻳﺆﻣﻦ ﺑﻔﺮﺿﻴﺘﻬﺎ ﻭﺗﺄﻛﺪﻫﺎ ﻭاﻟﻮﻋﻴﺪ ﻋﻠﻰ ﺇﺿﺎﻋﺘﻬﺎ ﺛﻢ ﻳﺘﺮﻛﻬﺎ ﻣﻊ ﺃﻧﻬﺎ ﻋﻤﻞ ﻳﺴﻴﺮ ﺳﻬﻞ ﻣﻮﺯﻉ ﻓﻲ اﻟﻴﻮﻡ ﻭاﻟﻠﻴﻠﺔ ﻭﻻ ﻳﺘﺮﻛﻬﺎ ﺇﻻ ﺃﺣﺪ ﺭﺟﻠﻴﻦ: ﺇﻣﺎ ﺷﺎﻙ ﻓﻲ ﻓﺮﺿﻴﺘﻬﺎ، ﺃﻭ ﻣﻌﺎﻧﺪ ﺃﻋﻈﻢ ﻋﻨﺎﺩ ﻟﻠﻪ ﻭﺭﺳﻮﻟﻪ.

Akajibu kwa kusema:

Swala nafasi yake ni kubwa na jambo lake ni kubwa, na ndio nguzo ya muhimu zaidi ya Uislamu baada ya shahada mbili kwa makubaliano ya wanazuoni wote, na yamekuja makemeo makali juu ya kuipoteza, katika Qur-an na Sunnah, na sidhani kama kuna yeyote anaeamini ufaradhi wake, na mahimizo yake na makemeo yake juu ya kuipoteza, kisha anaiacha pamoja nakuwa ni amali ndogo nyepesi aliyogawanywa katika usiku na mchana, na hakuna anaeiacha ispokuwa ni mmoja kati ya watu wawili: Ima ni mtu mwenye shaka juu ya ufaradhi wake, au ni mpingaji upingaji mkubwa wa Allah na Mtume wake ﷺ.


🔸ﻭﻣﻦ ﺯﻋﻢ ﺃﻧﻪ ﻣﻘﺮ ﺑﻮﺟﻮﺑﻬﺎ، ﺃﻭ ﻗﺎﻝ ﺇﻧﻪ ﻣﻘﺮ ﺑﻮﺟﻮﺑﻬﺎ ﻭﻟﻜﻨﻪ ﻟﻢ ﻳﺼﻞ ﻓﻬﻮ ﻛﺎﻓﺮ ﻭﺇﻥ ﻛﺎﻥ ﻳﺼﻮﻡ ﻭﻳﺤﺞ ﻭﻳﺰﻛﻲ

Na atakaedai kuwa anakiri uwajibu wake, au akasema kuwa anakiri uwajibu wake, lakini haswali, basi huyo ni kafiri, hata kama atakuwa anafunga, anahiji, na anatoa zaka.


❶ ﻟﻘﻮﻝ اﻟﻨﺒﻲ ﺻﻠﻰ اﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ: "ﺑﻴﻦ اﻟﺮﺟﻞ ﻭﺑﻴﻦ اﻟﺸﺮﻙ ﻭاﻟﻜﻔﺮ ﺗﺮﻙ اﻟﺼﻼﺓ"

ﺭﻭاﻩ ﻣﺴﻠﻢ.

Kwa mujibu wa kauli ya Mtume ﷺ: 

[Kitenganishi baina ya mtu na shirki na ukafiri ni kuacha Swalah]

Ameipokea Muslim.


❷ ﻭﻗﺎﻝ: "اﻟﻌﻬﺪ اﻟﺬﻱ ﺑﻴﻨﻨﺎ ﻭﺑﻴﻨﻬﻢ اﻟﺼﻼﺓ ﻓﻤﻦ ﺗﺮﻛﻬﺎ ﻓﻘﺪ ﻛﻔﺮ"

ﺭﻭاﻩ اﻟﺨﻤﺴﺔ.

#Tutekeleze_Swala_nduguzangu.✅️