SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 30 Machi 2017

T media news

Rais Magufuli ateua kamati ya wataalamu kuchunguzi makontena ya madini yanayoshikiliwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 29 Machi, 2017 ameteua kamati ya wataalamu watakaofanya uchunguzi kwa lengo la kubaini kiwango cha madini kilichomo katika makontena yenye mchanga wa madini yanayoshikiliwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kamati hiyo yenye wajumbe 8, inatakiwa kuanza kazi haraka iwezekanavyo.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni;

Abdulrahman Hamis MrumaJustianian Rwezaura IkingulaJoseph BushweshaigaYusuf NgenyaJoseph Yoweza PhilipAmbrose ItikaMohamed Zengo MakongoroHery Issa Gombela

Wajumbe wote wa kamati hii wanatakiwa kufika ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam Ijumaa tarehe 31 Machi, 2017 saa 4:00 asubuhi.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

29 Machi, 2017