Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta amewapongeza wachezaji wenzake kwa ushindi walioupata wa magoli 2-1 dhidi ya Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa kwenye uwanja wa taifa Jumanne March 28, 2017.
Samatta ambaye hakuwepo kwenye mechi hiyo alitweet kwenye account yake ya twitter (@samatta77) kuwapongeza wachezaji wenzake kwa kupata ushindi na akawatania kwamba zawadi yao wanywe soda hala yeye atalipa.
“Hongera Stars, kunyweni soda wote bili juu yangu,” ndivyo unavyosomeka ujumbe wa mshambuliaji huyo ambaye aliifungia Stars magoli mawili ilipoichapa Botswana 2-0 kwenye mechi ya kirafiki.
Samatta aliondoka Jumatatu usiku kwa ruhusa maalum ya benchi la ufundi la Stars chini ya kocha Salum Mayanga akiwa anawahi majuku kwenye klabu yake ya KRC Genk.
Aidha Mayanga alisema, mchezo wa jana alipanga kutumia zaidi wachezaji wa ndani kwa sababu ya maandalizi ya michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa Afrika wanaocheza ligi za ndani (Afrika).