SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 29 Machi 2017

T media news

Noma Sana ..Watuhumiwa wa Ugaidi Waitisha Mahakama,Watoa Masharti Haya Makubwa..!!!


Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana imesikiliza malalamiko ya watuhumiwa 61 wanao kabiliwa na kosa la ugaidi, ambapo ni shauri lililofunguliwa mwaka 2014.

Wakizungumza  mahakamani hapo watuhumiwa hao wamesema kuwa jana ndiyo itakuwa mwisho wao kufika kwenye viwanja vya mahakama hiyo mpaka upande wa jamuhuri utakapo kamilisha upelelezi wao.

Wamesema wamekuwa wakifika mahakamani kwa muda ambapo wengi wao familia zinateseka na kusambaratika sababu ya kukaa mahabusu kwa miaka minne kwa makosa ya kusingiziwa.

Aidha wamesema wamekuwa wakipewa ahadi  hewa na mkuu wa upelelezi  kuwa angeshughulikia shauri hilo ndani ya miezi mitatu na kwamba suala la mahakama kushindwa kutekeleza wajibu wake  wa kikatiba linaleta ukakasi kwa wananchi.

Hakimu Mfawidhi Nestory Baro wa mahakama hiyo amewataka watuhumiwa kuwa na subira wakati wakishughulikia shauri lao ambapo kesi itatajwa April 11 mwaka huu na amewataka kufika mahakamani siku hiyo bila kukosa wakati akifanya utaratibu wa kumtafuta mkuu wa upelelezi na kuzungumza naye