GWIJI wa Cameroon, Rigobert Song amerejea nyumbani baada ya matibabu ya kupooza Ulaya.
Song amekuwa Ufaransa tangu Oktoba mwaka 2016 ambako alipelekwa baada ya kupata ugonjwa wa kupooza.
Ndege iliyombeba gwiji huyo ilitarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Younde juzi.
Song mwenye umri wa miaka 40 aliruhusiwa katika hopitali La Pitie Salpertriere nchini Ufaransa baada ya matatizo yake.
Wadau mbalimbali wa soka waliguswa na tukioa hio na ulimwengu wa soka uliguswa na tukio hilo na kumfariji mchezaji huyo aliyecheza mechi 137 timu ya taifa ya Cameroon kushinda Medali moja ya dhahabu ya Olimpiki mwaka 2000.
Song amecheza klabu kadhaa England zikiwemo Liverpool na West Ham. Kabla ya kuanza kuumwa alikuwa akifanya kazi kama kocha Cameroon kuftia kuachia ngazi s Chad.