SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 29 Machi 2017

T media news

Mambo matano ya kufanya kumfurahisha mpenzi wako

Kama wewe uko katika mahusiano na unataka kuyafanya yakue, ni vyema ukayachukulia hatua baadhi ya mawazo yanayoweza kufanya penzi lenu kuwa imara, lenye furaha na kujenga uaminifu kati yenu. Haya hapa ni mamo matano muhimu ambayo unaweza kuyafanya ili kumfanya mpenzi wako awe na furaha wakati wote:

Msikilize.

Wanawake wanapenda sana kusikilizwa, na unapotenga muda wako kumsikiliza huwa anahisi unamjali sana na hupata furaha. Japo wanaume wengi hawapendi kusikiliza, lakini inabidi ujitahidi kuwa karibu na mpenzi wako na utenge muda mzuri wa kumsikiliza.

Mnunulie zawadi za aina mablimbali.

Kama umezoea kumpa mpenzi wako zawadi za aina moja, mfano kumnunulia kadi kila anaposheherekea siku yake ya kuzaliwa, basi yahitaji ubadilike. Jaribu kusikiliza baadhi ya tarifa anazozitoa kuhusu vitu anavyopendelea, na anavyopenda kupokea. Jaribu kupata msaada wa kujua anapendelea nini kutoka kwa rafiki zake. Kumpatia mpenzi wako vitu anavyovipendelea zaidi kutalihuisha penzi lenu na kulifanya lionekane jipya tena.

Jitahidi kuwa karibu na marafiki zake.

Kitu cha msingi kufanya kwa muda wote ambao umekuwa katika mahusiano na mpenzi wako, jaribu kuwazoea rafiki zake. Jitahidi kuwa kuwazoea wale watu wa karibu naye. Huhitaji kuwazoea marafiki zake wote. Hii itakusaidia kumjua mpenzi wako zaidi na kujenga urafiki wenu.

Penda na thamini vitu anavyovipenda.

Kama mpenzi wako anapendelea vitu ambavyo wewe huvipendi, jitahidi kumuonyesha kuwa unavifurahia. Siyo lazima uvipende lakini unaweza kumsifia pale anapovifanya. Kuheshimiana ni chachu ya mafanikio katika  mahusiano, hivyo kama wewe umekuwa ukichukulia kana kwamba maslahi yake ni madogo, ni wakati wa kuanza kuonyesha kuwa unathamini baadhi ya vitu anavyovipendelea. Hii itamfanya ajisikie kuwa anapendwa na itaimarisha penzi lenu.

Tumieni wakati mwingi pamoja.

Mnapokuwa katika mahusiano ni muhimu kutenga muda wa kuwa na mpenzi wako. Mfano siku za weekend hakikisha unamtembelea ama mnakwenda maeneo kama vile maktaba, mghahawani, kwenye bustani za mji, ufukweni na maeneo mengine mbalimbali ambayo hamjawahi kuyatembelea. hii itawajengea ujasiri na kuaminiana katika mahusiano yenu.