SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 29 Machi 2017

T media news

Fahamu njia bora ya kutumia likizo yako ya kazi

Zaidi ya nusu ya wafanyakazi wengi huwa hawatumii muda wao wote wa likizo, na huwa wanakosa vingi zaidi ya furaha na kupumzika. Utafiti uanonyesha kuwa kupata muda wa kupumzika kuna faida kiafya. kupumzika mara kwa mara hukusaidia kupunguza mawazo, kupunguza uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo, kuongeza ufanisi kazini na vilevile hukufanya kuwa karibu na familia yako.

Unawajua wasiosumbuka kutumia muda wao mwingi kutalii? Familia ya Kardashians inajulikana sana duniani kwa safari zao za kifahari katika maeneo tofauti tofauti ulimwenguni. Huwa wanatumia gharama kubwa sana katika matembezi yao kama kukodisha jumba la ghorofa lililokombele ya ufukwe wa bahari huko Costa Rica kwa gharama ya dola za kimarekani 17000 na magari ya kifahari kama Rolls Royce

Itazame video hii na ujifunze mengi kuwahusu Kim, Khoe na kundi lao wanavyotumia muda mwingi wakiwa mbali na nyumbani. Japo yawezekana huwezi kugharamia safari za likizo za gharama kama wao, ila kuona tu namna wanavyofurahia inaweza kukuvutia na wewe siku moja uombe likizo ya siku chache kutoka kwa bosi wako