Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limeitisha majadiliano kuhusu hali ya uchumi wa nchi inavyokwenda na kupelekea wafanyakazi kwenye makampuni mengi kupoteza ajira zao kutokana na kushindwa kulipwa stahiki zao.
Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya alisema kuwa watafanya mkutano wa siku mbili na wadau kuhusu hali ya uchumi kujadiliana njia na hatua za kuchukuliwa ili kuzia watu kupoteza ajira zao hasa kwenye sekta binafsi.
Wakati hayo yakiendelea, Tanzania Distilleries Limited ambayo ni kampuni tanzu ya Tanzania Breweries Limited imetangaza kupunguza wafanyakazi wake wasiozidi 50 ili kuweza kukabiliana na hali ya kiuchumi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 27 na kampuni hiyo, wale wote watakaoathiriwa na uamuzi huo wataliwa stahiki zao zote.