Ni hakika kwa100% Daud Albert Bashite alimaarufu Paul C. Makonda amekiri tuhuma zote mbele ya Kamati ya Bunge leo,
Kinachosubiriwa ni maoni ya kamati hiyo kwenda kwenye Bunge ambapo taarifa na maoni hayo vitasomwa Bunge linaloanza wiki ijayo 04/04/2017.
Mimi kama raia mwenye haki na wajibu kwa taifa langu, nikitambua haki yangu kwamba Bunge ni chombo changu cha uwakilishi, Natoa onyo kwa Kamati husika na Bunge pia, Ole wenu mje na hadithi ya kwamba MMEMSAMEHE.
Narudia ole wenu, Ole wenu, ole wenu kabisa..... Sisi wananchi tuna kesi nzito sana na huyu mtu nje ya yeye kutudharau na kutudhihaki kupitia bunge letu ambalo nyinyi tumewatuma mtuwakilishe...
Nataka mtambue kila mnachofanya hamfanyi kwaniaba yenu, bali kwaniaba yetu, Hivyo sisi tuliowatuma tayari tulishamhukumu na kufunga file lake.
Ole wenu mbadilishe maamuzi ya umma, Sisi ndio wenye mamlaka ya mwisho katika nchi hii, sio rais, sio jaji, sio spika, bali sisi tukisema na kuamua mbinguni na duniani tumeamua.... Hii ni kwamjibu wa katiba ya 1977 na ile inayopendekezwa ya Warioba na hata ile ya Marehemu Sitta bado hazikutung'anya mamlaka yetu.
Ukisikia kwamba mamlaka yote yanatoka kwa Mungu haimaanishi Mungu wa ulaya au asia, Mungu ni sisi Watanzania..
Sisi tukisema ni Mungu amesema!
Ole wenu wabunge!!!!!
Na Yerico Nyerere