SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 29 Machi 2017

T media news

Kwenye Sakata la Mchanga wa Dhahabu: Huu Ndio Ukweli wa Ndani Jinsi Rais na Spika Walivyodanganywa..!!!


Naomba ni declare interest kuwa, mimi ni mmoja wa wataalam wanaouhusika na ishu iyo ya mchanga.

Kifupi naomba nieleze kile ambacho kipo kwenye makontena. Kilichopo kwenye makontena kwa asilimia kubwa ni copper(Cu) , ifufuatiwa na silver (Ag) na dhahabu (Au) haizidi asilimia 0.05.

Yule Afisa wa Bandari aliyesema kuwa zaidi ya asilimia 90 ni dhahabu ni muongo na anapaswa kuiomba radhi ACACIA na watanzania kwa ujumla na atumbuliwe kwenye nafasi yake.

Kiwango kilichopo kwenye yale makontena zaidi ya 256 ni kati ya sililimia 0.012 -0.02, g/t

Mh spika alidhani kiwango cha asilimia 0.02 kuwa ni kidogo na hauwezi kupata faida iwapo utalisafirisha kontena kutoka mgodini mpaka China, Japan au Ujerumani.

Naomba nimuulize, anajua gharama ya kusafirisha hilo kontena? Kifupi haizidi milioni 8.

Nikija kwenye mchanganua wa hiyo asilimia 0.02 kwa contena, naomba nimfafanulie mh spika kama ifuatavyo:-

(1) 0.02% hii ni gram kwa tani, kwa maana hiyo hii ukiizidisha kwa tannage zilizopo (eg 20.5tn), utapata 0.41%.

(2) Hii 0.41 ili upate ppm, unatakiwa uizidishwa kwa 10000, utapata 4100ppm au g/t.

kwa maana nyingine, yule mtaalam wa TMAA aliwaambia kwenye kila container kuna takriban kilo 4.1. sasa hii ni ndogo?

(3) Kwa sasa kilo ya dhahabu ni takribani mil 90. 90x4=360m.

sasa iwapo utasafirsha container moja kwa 10m, huoni kuna faida?

Pia Kamati ya Bunge kupitia Spika alidai kwa mwaka ACACIA, Buzwagi na Bulyanhulu huzalisha takribani idadi ya makontena elfu 50, na kwa maana hiyo contena milioni moja yameisha safirishwa. HUU SIO UKWELI.

Ukweli ni kwamba hizo ni tani za mchanga wa dhahabu na sio idadi ya kontena.

Mpaka sasa, migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi wameisha safirisha makontena yasiozidi elfu 50.

Mpaka sasa Bulyanhulu peke yake wamesafirisha contena sizizozidi elfu 42. Sasa hizo contena 1m, zimetoka wapi?

Mh. rais kuna wanakupotosha, na hili utalithibitisha kupitia sample zilizochukuliwa na Mh Waziri Mkuu jana katika mgodi wa Buzwagi, kwani kati ya makontena aliyochukua sample, moja wapo ni kontena ambalo lililkua na seal na document zote za serikali na lilikua tayari kusafirishwa kwenda Ujerumani. Baada ya tamko la rais kontena hilo lilirudishwa mgodini pamoja na makontena mengine 3, yakiwa tayari yamefika Isaka.

My take:-

Kwenye hili sakata la mchanga, mihemuko isitumike. Wawekezaji wa ACACIA hawamuibii mtu kwani hata kama kungekua na 90% ya dhahabu, TMAA huchukua sample pia, kiasi kwamba wangeweza kuiambia serikali kuwa ACACIA wanawaibia kwa kutoa takwimu za uongo.

Iwapo mikataba haiwafaidishi watanzania, ifanyiwe review kwani ACACIA hutumia mikataba hiyo hiyo kufanya calculation zao.

Iwapo itathibitika kuwa ACACIA pia hawawaibii watanzania kwa kuficha dhahabu kwenye mchanga, basi pia Katibu Mkuu aombwe radhi.