Shirikisho la soka duniani FIFA March 28, limetangaza kumfungia mechi 4, nahodha wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya FC Barcelona ya Hispania, Lionel Messi kwa kosa la kutoa maneno machafu kwa mwamuzi katika mchezo dhidi ya Chile,Machi 24.
Messi alipewa kifungo hicho saa sita kabla ya mchezo dhidi ya Bolivia. Pia amepigwa faini ya Paundi 8,100.
Messi alionekana kukasirika katika mchezo huo dhidi ya Chile baada ya mwamuzi msaidizi Marcelo van Gasse kuinua kibendera akiashiria mchezaji huyo kumfanyia madhambi mpinzani. Messi alirusha mkono wake juu na kumbwatukia mwamuzi huyo kwa kusema ‘la concha de tu madre’, kwa tafsiri ya “f*** off, your mother’s ****’ . .
Baada ya mchezo kumalizika kwa Argentina kushinda 1-0 kwa goli la Lionel Messi, nahodha huyo alikataa kumpa mkono mwamuzi huyo msaidizi.
Na hizi ndio mechi ambazo atakosa Messi ni zile za ushindani ambazo zote ni za kufuzu kombe la Dunia.
Mechi hizo ni
March 28 – Bolivia (A)
August 28 – Uruguay (A)
September 5 – Venezuela (H)
October 2 – Peru (H)