Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewasili bungeni mjini Dodoma leo asubuhi na kupokelewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Bunge ikiwa ni kuitikia wito wa Bunge wa kumtaka kufika mbele ya kamati.
RC Makonda amepokelewa na Owen Mwandumbya ambapo aliitwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge akitakiwa kujieleza kuhusu kauli aliyoitoa inayodaiwa kuwa ni ya kulidharau na kulikashifu kwa wabunge.
Akitoa hoja katika mkutano wa bunge uliopita, Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara alisema kuwa viongozi mbalimbali hasa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kiasi cha kuingilia majukumu yasiyo yao, na wakati mwingine kuingilia majukumu ya Bunge, na kutolea mfano Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Alexander Mnyeti.