SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 31 Machi 2017

T media news

Hali Mbaya CCM Yawaliza Makatibu Wakuu...!!!


Viongozi wa CCM mkoa wa Morogoro wamewataka makatibu wa matawi na mashina wa chama hicho kuachana na mpango wa kususia uchaguzi wa viongozi wa ngazi hiyo kwa madai ya kutokulipwa posho za kusimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake jana, Katibu wa Tawi la Luleni, Kata ya Tomondo, Salumu Waziri alisema kutokana na kudai posho hizo kwa muda mrefu ameamua kususia uchaguzi huo na tayari amekabidhi fomu za wagombea kwenye ofisi ya kata.

Waziri alisema chama hicho kilitoa fedha za posho na kumkabidhi kiongozi mmoja wa wilaya ambaye hakuwalipa.

Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Kulwa Milonge alisema chama hicho kilishatoa fedha za kuwalipa viongozi wa matawi na mashina kupitia kwa katibu wa wilaya hiyo.